Latest Posts

Photostream

Newsletter

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every month.

  • By Platinum credit
  • Posted April 24, 2018

WAFANYAKAZI WA PLATINUM CREDIT WAPIGWA MSASA

Katika kuboresha huduma zake Platinum credit imewapatia wafanyakazi wake wa kitengo cha huduma kwa wateja mafunzo ya siku mbili, mafunzo hayo yameanza mapema leo tarehe 20/04/2018 Jijini Dar es salaam na kutarajiwa kumalizika tarehe 21/04/208.

Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo Lazarus Kithuku aliwataka wafanyakazi hao wafatilie mafunzo hayo kwa umakini mkubwa na watambue kuwa kila kitu kinachofundishwa ni cha muhimu na kitawasaidia katika majukumu yao ya kila siku.

Mnatakiwa kuwa makini na kuhakikisha mnaelewa kila kitu kinachofundishwa hapa, kwani vyote ni vya umuhimu na vitaongeza ufanisi na weledi katika utendaji wenu wa kazi

Mafunzo hayo yenye lengo la kuongeza Ufanisi katika kazi yaliongozwa na Robert Mubisa kutoka Kenya akishirikiana na Newton Edward wa Tanzania.