Latest Posts

Photostream

Newsletter

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every month.

  • By Platinum credit
  • Posted April 24, 2018

PLATINUM YAJITOA TENA KUWAKUMBUKA WATOTO WA MAZINGIRA MAGUMU

Ukiacha kazi na majukumu yetu ya kila siku ya kutoa huduma za kifedha kwa jamii, pia tunayo desturi ya kusaidia jamii inayotuzunguka katika nyanja mbalimabali zikiwemo huduma za kiafya, elimu, miundo mbinu, na kusaidia wenye uhitaji maalum pale inapotupasa. Mwishoni mwa wiki iliyopita(17/03/2018) tulitembelea kituo cha watoto yatima Mazizini katika mkoa wa Mjini Magharibi, Tanzania visiwani (Zanzibar) na kuwapatia baadhi ya mahitaji muhimu watoto wa kituo hicho yaliyojumuisha madaftari, vitambaa vya sare za shule, mafuta yakupikia, sukari, mchele, unga na sabuni za kufulia.

Platinum Credit inapenda kutoa wito kwa jamii na Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji kwa kadiri Mungu anavyowajalia kwani hata vitabu vya dini vinasema kutoa ni Moyo